Tanzania Kuwa Nchi kwanza Duniani Kutumia Kitambaa Kilichowekewa viatilifu Kudhibiti Malaria.
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kufanya majaribio ya kupambana na mbu waenezao magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria kwa kutumia kitambaa kilichowekewa viatilifu ili kudhibiti ugonjwa malaria ambao ni tishio kwa afya ya wananchi wengi wanaoishi vijijini. Hatua hiyo ya utafiti imefikiwa na watafiti wa magonjwa ya binadamu katika cha taifa cha Magojwa ya Binadamu (NIMR) katika kituo cha Amani mkoani Tanga ili kuweza kuwadhibiti mbu waenezao ugonjwa malaria ambao unaathiri watu wa rika zote nchini. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo. Katika kufanikisha majaribio hayo, Dkt. Kisinza amesema kituo hicho kinaendelea vizuri na majaribio a...