TCRA : Watumiaji Simu FEKI wazidi Kupungua Kutoka asilimia 30 hadi 13
Kadri siku ya kuzima simu feki kote nchini inavyokaribia imebainika kuwa wanaozitumia wanazidi kupungua nchini. Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy amesema tangu ilipotangaza mwaka jana kuwa itazima simu feki ifikapo mwishoni mwa Juni, idadi ya watumiaji imepungua kutoka asilimia 30 hadi 13. Alisema wakati wa uhakiki wa matumizi ya simu feki Desemba mwaka jana, mamlaka hiyo ilibaini kuwapo asilimia 30 ya simu bandia zinatotumika nchini. TCRA ilifanya uhakiki mwingine Februari ambao ulibaini matumizi ya simu feki kupungua hadi asilimia 18. “Uhakiki wa Machi ulibaini matumizi yameshuka zaidi hadi kufikia asilimia 13,” alisema Mungy na kubainisha kuwa TCRA itafanya tathmini nyingine kabla ya muda kumalizika. “Tunatumaini matumizi ya simu feki yataendelea kupungua. Hadi kufikia Juni mwishoni kusiwe na mtu anayetumia simu feki,” alisema Mungy. Meneja huyo alisema matokeo ya tathmini hiz...