Amtaka Mama yake Amtunzie Watoto Baada ya Kumuua Mkewe kwa Kumchinja na Kisha na Yeye Kujinyonga
Watu watatu wamefanya mauaji ya kutisha, wawili wamechinja wake zao, huku mmoja akiacha ujumbe wa kumtaka mama yake mzazi amtunzuie watoto na mwingine amemuua mama yake. Katika tukio la Dodoma, Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake. Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,” alisema. Katika tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua mama yake mz...