Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuweka mishahara ya watumishi hewa, kurejesha fedha hizo serikalini ; au kubainisha waliokuwa wakitumia akaunti hizo, kuchukua fedha. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makonda alisema benki ndio pekee wanaoweza kusaidia mkoa, kutambua wahusika waliokuwa wanatumia akaunti hizo pamoja na wale waliokuwa wanachukua fedha hizo. Alisema watu hao wasipopatikana, inamaanisha fedha bado zipo katika benki hizo, hivyo zinapaswa kuzirudisha serikalini zifanye maendeleo kwa wananchi. “Tayari tumeshaziandikia benki hizo barua na kuwapatia majina na akaunti na kuwataka kutuwasilishia majina ya wahusika, waliohusika na akaunti hizo ili kusaidia kutambua mtandao mzima wa wahusika wa suala la watumishi hewa ambao wameigharimu serikali,” alisema Makonda. Alitaja benki hizo pamoja na fedha wanazodai kuwa ni benki ya NMB ambayo inadaiwa zaidi ya Sh bilioni mbili, CRDB zaidi ya mili...