Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kigwangalla Avifungia Vituo vya Tiba Asili zitolewazo na Kiliniki za Kikorea

Kigwangalla Avifungia Vituo vya Tiba Asili zitolewazo na Kiliniki za Kikorea

Picha
SERIKALI imesitisha huduma za tiba asili zitolewazo na Kiliniki za Kikorea, Maibong Sukidar Medical na Korea Medical Clinic zilizopo Jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutokuwa na kibali kwa zaidi ya miaka nane pia kuchanganya tiba asili na za kisasa na mbadala bila ya idhini kutoka baraza la usajili la tiba asili nchini Hatua ya kufungwa kwa kliniki hizo imechukuliwa jana baada ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kufanya ziara ya kushtukiza kukagua  vibali na huduma zitolewazo katika kiliniki hizo. Kigwangalla alizitaja sababu zilizopelekea kufungwa kwa Kiliniki ya Korea Medical kuwa ni pamoja na  Kutibu magonjwa ambayo haikupewa kibali kutoka serikalini na kuhifadhi dawa ambazo hazihusiani na magonjwa inayotibu “Kliniki hii ninaamuru ifungwe kwa makosa matano ikiwemo kosa la kuchanganya tiba asili na kisasa, kutokuwa na kibali, usajili halali, matabibu wake hawajui lugha ya Kiswahili na au kiingereza, usajili ulimt...