Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya 2016

Rais Magufuli Akutana Na Waziri Mkuu, Jaji Mkuu Na Kamishna Mkuu Wa TRA Ikulu Jijini Dar Es Salaam Mei 23,2016

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Alphayo Kidata Ikulu jijini Dar es Salaam

Picha Mbalimbali za Rais Magufuli Alivyoshiriki Ibada Ya Jumapili Ya Kupaa Kwa Bwana Katika Parokia Ya Toleo La Bwana Jimbo La Arusha Mjini Mei 08,2016

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Mei, 2016 ameungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwana iliyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio. Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana. "Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha"  amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo. Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa ...

Rais Magufuli Akutana Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Tatu Benjamin Mkapa Pamoja Na Mjumbe Maalum Wa Rais Wa Guinea Bisau Februari 25,2016

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 25,2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Genarali Omar Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz Ikulu jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mjumbe huyo alileta salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Guinea Bisau. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua kutoka Genarali Omar Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea Bissau Jose Mario Vaz. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mjumbe Maalum wa Rais wa Guinea B...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Uingereza ya Leo Alhamisi Ya February 25, 2016

Picha