Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kubenea Akana Kumtukana Paul Makonda....Kesi Yaahirishwa Hadi March 10

Kubenea Akana Kumtukana Paul Makonda....Kesi Yaahirishwa Hadi March 10

Picha
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hakutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kama inavyodaiwa. Kubenea alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa utetezi huku akiongozwa na wakili wake, Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. “Mimi sijasema hayo maneno kuwa Makonda ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe cha kupewa, bali nilimwambia wewe umeteuliwa na Rais na mimi nimechaguliwa na wananchi,” alidai. Kubenea aliendelea kudai kuwa Desemba 14, 2015, katika kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda hicho, alimwambia Makonda hawezi kufunga mkutano bila ya yeye kuzungumza kwa sababu ni mwakilishi wa wananchi. Alidai kuwa Makonda alimjibu kila alipokuwa akizungumza kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho kwa kuwa ni rais wa Kinondoni.  “Nilimjibu na mimi ni mbunge, nimeteuliwa na wananchi, lazima aheshimu uwapo wangu pale,...