Madiwani wa Chadema Wilayani Hai Wasusa Kuhudhuria Kikao cha Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadiki
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Helga Mchomvu, wamesusa kuhudhuria kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki wakati akizungumza na viongozi wa vitongoji, vijiji, kata, viongozi wa taasisi za serikali na dini. Sadiki alifika wilayani Hai jana, ikiwa ni moja ya ziara zake katika wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kuzungumza na viongozi mbalimbali wanaowakilisha wananchi, pamoja na kusikiliza kero zinazozikabili wilaya hizo. Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Hai Mjini, madiwani hao ambao wote ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hawakuonekana hata mmoja huku eneo walilokuwa wameandaliwa likibaki na viti vilivyo wazi. Awali, Mkuu wa Mkoa alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa lengo la kupokea taarifa ya wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mchomvu aliwasili kwa kuchelewa na muda ulipofika wa k...