UMUHIMU WA KITUNGUU MAJI KWENYE MWILI WA MWANADAMU
Na Zuhura Simba Kitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi. Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha. Anaeikitumia kitunguu maji ajihadhari kukitumia baada ya kukihifadhi kikiwa kimekatwakatwa, kwasababu hufanya oksaidi (oxide) na huwa kiini chenye sumu. Kwa hivyo yatakiwa kitumiwe kikiwa fresh. Imethibitiswa kisayansi kuwa juisi yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua-kikuu, huuwa baada tu ya kunusa moshi wake. Nchi mashuhuri duniani katika upandaji wa kitunguumaji ni Misri (Egypt). Razi amesema: “Kitunguu maji kikifanyiwa achari, ukali wake hupungua na hutia nguvu maida, na kitunguu kilichofanywa achari, hufungua mno hamu ya kula” Kwa ajili hiyo watu wa misri hula ktunguumaji kikiwa kimechomwa, hutia nguvu mwilini, huufanya uso kuwa mwekundu na huimarisha misuli. Ibn Baitar amesema: ” Kitunguu maji hufungua hamu ya kula, hulainisha tumbo. Kikipikwa hukojoza na huzidisha nguvu za kiume kikichemshwa. Na kinachokata harufu ya kitunguumaji ni lozi (almond)....