Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Sakata la Sukari: Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea Walaji Tanzania (TCSA) Atoa Tahadhari

Sakata la Sukari: Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea Walaji Tanzania (TCSA) Atoa Tahadhari

Picha
Wakati Serikali ikiendelea kuwaadhibu wafanyabiashara wakubwa kwa madai ya kuficha sukari katika maghala, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea Walaji Tanzania (TCSA), Benard Kihiyo amesema hatua za kuwasaka ni nzuri lakini itaharibu usambazaji na upatikanaji wa bidhaa hiyo. Kauli ya Kihiyo imekuja wakati msako dhidi ya wanaoficha sukari ukiwa umepambamoto. Jana, mfanyabiashara wa Arusha, Romanus Macha alisalimisha tani 33 za bidhaa hiyo serikalini. Akizungumza baada ya kutembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Arusha, Macha alisema ameamua kusalimisha sukari hiyo ikiwa ni kufuata agizo la Serikali. Alisema alitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa na wa wilaya kuwa ana sukari. “Mfuko wa kilo 50 nilinunua kwa Sh90,000, nilitegemea kuuza Sh92,000. Kwa kuwa nimeshaisalimisha nasubiri bei elekezi ya Serikali,”  alisema Macha. Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Daniel Machunda alisema maofisa wake hawakukuta dosari kwenye sukari hiyo lakini wanasubiri ripoti ya...