Madaktari Wawili na Muuguzi Wasimamishwa Kazi Kwa Kumtolea Lugha Chafu Mjamzito Aliyejifungulia Chooni
Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala imewasimamisha kazi madaktari wawili na muuguzi mmoja, kwa madai ya kumtolea lugha isiyostahili mjamzito Asha Said (17), aliyejifungulia chooni. Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita katika hospitali hiyo, baada ya Asha kujifungulia chooni na madaktari na wauguzi hao kumtolea lugha chafu, bila kuelezwa sababu za kufanya hivyo. Mganga Mkuu wa Amana, Dk Meshack Shimwela alisema jana kwamba watumishi hao ambao hakuwataja wamepelekwa katika Baraza la Watumishi na Madaktari la hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi. “Kilichotokea siku ile ni kauli zilizotoka kwa watumishi hao kwenda kwa mama aliyejifungua, ambaye pia alikuwa mdogo kiumri. “Sisi madaktari na waaguzi tuna taratibu za kinidhamu, huwa tunazifuata baada ya watumishi kubainika kufanya makosa, hatua ya kwanza ndiyo hiyo tusubiri nyingine wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao,” alisema Dk Shimwela. Dk Shimwela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), ...