MAKALA YA SHERIA: JE UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI MJINI, FUATA UTARATIBU HUU
Na Bashir Yakub. Tunapoongelea upimaji ifahamike kuwa upimaji upo wa aina nyingi.Kutokana na hilo upimaji unaoongelewa hapa ni upimaji miliki. Lakini pia tunaongelea upimaji miliki wa ardhi mijini na sio vijijini. Upimaji wa ardhi miliki ni upimaji ambao lengo lake ni kummilikisha mtu ardhi. Kummilikisha mtu ardhi sio kumuuzia ardhi. Kummilikisha mtu ardhi ni kutambua ardhi yake kimipaka na kumpatia nyaraka mahsusi(specific) inayohusiana na umiliki( hati). Kwa maana hii wanaomiliki ardhi ambazo hazijapimwa hatuwezi kusema wamemilikishwa ardhi . Haijalishi ardhi hizo ni za kwao na ...