Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Benki Kuu ya Tanzania yawaka moto

Benki Kuu ya Tanzania yawaka moto

Picha
Benki Kuu ya Tanzania yawaka moto Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Najuwa wajuwa, Lakini mimi nakujuza zaidi ASUBUHI ya Julai 5, 1984, wakazi wa Dar es Salaam waliamka kwa mshangao baada ya kusikia na kuliona jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) likiwa linaungua kwa moto uliokuwa umesambaza moshi mkubwa na mzito juu ya anga la mji  huo ulio ufukweni mwa Bahari ya Hindi. Tukio hilo lilitokea kiasi cha miaka 32 iliyopita, wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo, kama kawaida, Watanzania waliokuwa na kazi na ambao hawakuwa na kazi,  walifurika maeneo jirani ya jengo hilo ambalo ndilo ‘mama wa fedha’ za nchi hii na kushuhudia likiwaka moto huku magari kibao ya zimamoto na wafanyakazi wake wakihangaika kuudhibiti. Kama kawaida pia, majeshi ya usalama yalikuwa yamefurika eneo hilo ili kuhakikisha hapatokei purukushani yoyote wakati wa kupambana na janga hilo. Kwa ufahamisho tu ni kwamba jengo lililoungua ni lile  ‘orijino’, yaani je...