Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CCM Yawatupia Lawama Wakurugenzi Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar ......Yadai Wanawahujumu ili UKAWA Washinde

CCM Yawatupia Lawama Wakurugenzi Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar ......Yadai Wanawahujumu ili UKAWA Washinde

Picha
Wakati waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tamisemi na utawala bora George Simbachawene akitoa muda wa uchaguzi wa mameya kukamilika ifikapo machi 25 mwaka huu,Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba “Gadafi” amemuomba Waziri  huyo kuangalia upya  utendaji kazi wa wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni, akidai wamevuruga uchaguzi wa meya na naibu wake. Akizungumza na wanahabari jana, Simba alisema CCM imefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa wakurugenzi hao, ikiwamo kushindwa kutafsiri vyema vifungu vya sheria vilivyosababisha kuondolewa kwa majina ya wajumbe wao kwa madai kuwa hawana sifa za kushiriki uchaguzi huo. “Wakurugenzi hawakuwa majasiri katika kupambana na vitisho vya wajumbe wa Ukawa na kuwa wakweli. Walishindwa kutoa tafsiri sahihi ya wajumbe halali wanaotakiwa kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa jiji,” alilalamika Gadafi. Kwenye mkutano huo Gadafi alidai kwamba wakurugenzi hao walifan...