Serikali Yaondoa tozo ya uhakiki na Usajili wa Viwanda Vidogo Vidogo.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure. Prof Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya Wanawake Tanzania. Aidha amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi yetu. “Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake waanzE kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure.” Alisema Prof Mkenda. Pia alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi siku na kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka wafanye biashara kwa faida kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuonge...