Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Chanzo cha saratani ya matiti

Chanzo cha saratani ya matiti

Picha
Hakuna kitu kingine kizuri kama mwili wa mwanamke kwakuwa unaweza kuleta kiumbe binadamu kingine. Mwili wa mwanamke unazo ovari ambazo hutengeneza mayai na homoni maalumu ambazo hudhibiti mwili wake wakati wa ujauzito kuanzia wakati yai linaporutubishwa mpaka mwishoni mwa wastani wa miezi tisa (wakati wa kujifunguwa). Mfumo huu maalumu huanza kazi mara mwanamke anapoanza mzunguko wake wa uzazi (mzunguko wa hedhi). Kwa wastani kila siku 30 ovari zake zitazarisha yai na kuliweka katika mfumo wake wa uzazi likisubiri kurutubishwa. Wakati yai hili limetolewa, mwili wake utaanza kujiandaa kwa uwezekano wa kupata mtoto. Mfuko wa uzazi (uterus) utaanza kubadili uundwaji wake wa seli kwa kuandaa uwezekano wa kukishikilia kijusi (fetus) baada ya yai kurutubishwa. Wakati yai litakapokuwa limerutubishwa ovari zake (mwanamke) zitachukuwa majukumu ya mwili wake na kuhakikisha kuwa kijusi kinapata kile kinachokihitaji ili kuishi. Ubongo wa mwanamke pia huathiriwa kutokana na kutolewa kwa homon...