Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu wa Mkoa na Waziri Kitwanga Watofautiana Kuhusu Kuwepo Kwa Tawi la Magaidi wa Al Shabaab na Islamic State (IS) jijini Tanga

Mkuu wa Mkoa na Waziri Kitwanga Watofautiana Kuhusu Kuwepo Kwa Tawi la Magaidi wa Al Shabaab na Islamic State (IS) jijini Tanga

Picha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wametofautiana juu ya taarifa za kuwapo kwa tawi la kundi la kigaidi la Islamic State (IS) jijiniTanga Juzi, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) lilitangaza uwepo wa watu waliojitambulisha kuwa wawakilishi wa kundi hilo wanaoendesha operesheni kwa nchi za Afrika Mashariki. Shirika hilo lilieleza kuwa kundi hilo limetuma ujumbe na kujitambulisha kwa kutumia video ya dakika moja waliyoituma kwenye mtandao wa Twitter na kuzungumza na Waziri Kitwanga ambaye alithibitisha kuwa na taarifa hizo. “Tumezisikia na tumechukua hatua. Askari wetu wanafanya operesheni,” alikaririwa Waziri Kitwanga. Hata hivyo, jana Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwaambia waandishi wa habari, kuwa mauaji na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yaliyotokea mfululizo katika maeneo mbalimbali jijini hapa siku za karibuni hayahusiani na ugaidi. Alifafanua kuwa wahalifu waliopo huk...