Marcus Rashford: Shujaa Mpya Old Trafford Aliyevunja Rekodi ya George Best
Marcus Rashford alikuwa shujaa ambaye hakutabiriwa usiku wa Alhamisi dhidi ya FC Midtjylland, akifunga magoli mawili katika mechi yake ya kwanza ya kikosi cha kwanza katika ushindi wa 5-1 ambao uliiwezesha United kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-3 na sasa wanaelekea hatua ya 16 bora ya Europa League. Magoli hayo yalikuja wakati muhimu – na kuipa United uongozi wa 2-1 na kisha 3-1 na kubadili kabisa hali ya mchezo. Rushford alianza mchezo huo baada ya Anthony Martial kuumia wakati akipasha misuli – kabla ya usiku wa Alhamisi alikuwa hafahamiki, nje ya Manchester. Hivi ndio vitu 5 kuhusiana na shujaa mpya wa Old Trafford. 1. Asili Yake Rashford alizaliwa jijini Manchester mnamo mwaka 1997 na aliwahi kuitumikia Fletcher Moss Junior club, klabu ambayo iliwatengeneza akina Wes Brown, Danny Welbeck na wengine kama Tyler Blackett na Cameron Borthwick-Jackson. Rashford alijiunga na United na ametokea kwenye akademmi za Man United na kufanikiwa kuwakosha walimu wak...