Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CHADEMA Mkoa wa Dar es salaam watoa tamko

CHADEMA Mkoa wa Dar es salaam watoa tamko, wailaumu Televisheni ya Taifa kwa ubaguzi

Picha
Viongozi wa greater Dar Es Salaam wakati wa kikao na waandishi wa habari mapema hii leo wakitoa maazimio yao dhidi ya ubaguzi unaofanywa na kituo cha television ya TBC dhidi ya upinzani.  Makamu mwenyekiti Mwakyembe ametoa onyo kali na la mwisho kwa TBC maana ni chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za watanzania hivyo kiache kuendeshwa kwa minajali ya CCM tu.  Pia katika kikao hicho viongozi wa Dar es salaam kuu wameongelea zoezi linaloendelea chini ya serikali ya rais Magufuli la utumbuaji majipu na kubainisha ni kiini macho kwa watanzania. Akifafanua zaidi katibu Ndugu Kileo amesema anachofanya magufuli kwanza ni ukiukwaji wa sheria za nchi za ajira kazini ya mwaka 2004 lakini pia ni kinyume cha uongozi wa kidemokrasia ambapo kila mtu anahaki ya kusikilizwa na si maamuzi ya upande mmoja tu.  Zaidi Mh. Kileo amesema kinachofanyika ni kiini macho kwa sababu CCM inataka kujisafisha na uchafu huo wa jiji uliotendwa na Meya aliyepita ambaye ni mwanachama wa CCM Mh ...