Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya JEREMIAH JUMA and ELIUS MAGULI WAFUNGAJI BORA WAZAWA VPL

JEREMIAH JUMA & ELIUS MAGULI WAFUNGAJI BORA WAZAWA VPL, MGOSI & BARTHEZ…

Picha
Na Baraka Mbolembole Amis Tambwe ameshinda tuzo binafsi ya mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara 2015/16. Raia huyo wa Burundi amefunga jumla ya magoli 21. Mganda, Hamis Kiiza anafuatia katika chati hiyo baada ya kufunga magoli 19 na orodha ya wafumania nyavu watatu bora inafungwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye katika msimu wake wa kwanza VPL amefanikiwa kufunga magoli 17. Tatu Bora ya wafungaji haina mchezaji  raia wa Tanzania na badala yake majina yao yanaanzia katika nafasi ya nne ambako nyota wawili wa Taifa Stars, Elius Maguli wa Stand United ya Shinyanga na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons ya Mbeya wamefunga-kila mmoja amefunga magoli 14. Si haba hasa ukizingatia washambuliaji hao hawachezi katika timu za Yanga, Azam ama Simba ambako wanacheza Tambwe, Ngoma (Yanga) Kiiza (Simba.) Katika orodha ya wafungaji bora kumi wa kwanza, raia wa kigeni wamechomoza wanne tu hii inamaanisha kwamba hata wachezaji wazawa walifanya kazi nzuri katika ufungaji na wanastahili ku...