WASANII SHILOLE NA VANESSA MDEE WAMALIZA TOFAUTI ZAO
Inasikitisha kilichotokea mitandaoni kwa dada zangu wawili ninaowaheshimu sana kwenye muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammedi aka Shilole na Vanessa Mdee aka Vee Money. Usiku wa Jumanne ulikuwa ni wa furaha kwa wale wasiopenda maendeleo kwani walitumia msemo “vita vya panzi furaha ya kunguru” baada ya Shilole na Vanessa kutupiana maneno ya kukashifiana na kutishiana wakati kila mmoja akijua dhahiri hilo ni kosa kisheria. “Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliandika Shilole. Vanessa alijibu kwa kuandika: “ Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent.” Sitaki kuamini kuwa ki...