Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KUELEKEA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE: REKODI KALI ZINAZONYATIWA KUVUNJWA KATIKA USIKU WA MILAN

KUELEKEA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE: REKODI KALI ZINAZONYATIWA KUVUNJWA KATIKA USIKU WA MILAN

Picha
Na Eusebius Paul Kuweka rekodi mpya au kuifikia rekodi iliyowahi kuwekwa zamani na kuivunja kabisa ni jambo lenye furaha na fahari kubwa katika nyanja yoyote kimaisha. Lakini endapo kama utafanikiwa kuivunja rekodi hiyo katika mchezo wa fainali wa UEFA Champions League, sio rahisi kuufananisha msisimko wake. Ndani ya dimba la Giusseppe Meazza (San Sirro) Jumamosi hii kutakuwa na vita ya kuuwania ufalme wa Ulaya baina ya watoto wa mji mmoja, Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid umbali wa km 15 za barabara unaweka tofauti ya kimakazi baina ya mahasimu hawa. Wakati macho na akili za mamilioni ya mashabiki zikielekezwa katika kutaka kujua nani atakayeibuka na ushindi mwishoni mwa kipyenga cha mwamuzi Mark Clattenburg kutoka England, lakini zipo rekodi hizi kali ambazo wataalamu wangu hampaswi kukaa nazo mbali pindi zitakapokuwa katika hatihati ya kutumbuliwa. Magoli mengi kufungwa na mchezaji mmoja katika fainali ya UEFA Champions League Achana kabisa na mashindano ya hat-trick wan...