Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waarabu Waitupa nje AZAM Kombe la Shirikisho Barani Afrika...Waichapa Kipigo Kitakatifu

Waarabu Waitupa nje AZAM Kombe la Shirikisho Barani Afrika...Waichapa Kipigo Kitakatifu

Picha
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.  Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.  Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.  Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha,...