Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Lipumba Amvaa Rais Magufuli.....Asema Vitisho Vitaangamiza Uchumi wa Taifa

Lipumba Amvaa Rais Magufuli.....Asema Vitisho Vitaangamiza Uchumi wa Taifa, Ampigia Hesabu za Kiuchumi Duniani Kuhusu Sukari

Picha
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuchoshwa na utendaji wa Rais John Magufuli katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi. Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo jana mbele ya waandishi wa habari  katika Ofisi Kuu ya CUF iliyopo Buguruni, Dar es Salaam. Katika kukabiliana na changamoto za nchi hususani sekta ya uchumi, Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kutafuta ushauri sambamba na taratibu za kujenga uchumi wa soko shirikishi kutoka kwa Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu. Alisema, uzoefu wa Rais Mkapa wa kujenga utawala wa serikali unaweza kumsaidia kufanya uamuzi sahihi utakayosaidia wananchi badala ya kukagandamiza. Mchumi huyo alieleza kuwa, vitisho na ubabe wa Rais Magufuli vinaweza kuwaogopesha watendaji wake wakiwemo mawaziri na hivyo kushindwa kumueleza hali halisi na kwamba, kitendo hicho kinaweza kuathiri maendeleo ya nchi. “Kuna dalili kwa baadhi ya watendaji wa serikali hasa mawaziri, wakuu wa mikoa na wil...