CLEVELAND CAVALIERS YAUWAWA KINYAMA MBELE YA GOLDEN STATE WARRIORS. YAPOTEZAA MCHEZO WA PILI WA FAINALI.
Kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya fainali, Lebron James hakuwahi kupoteza michezo miwili mfululizo ya fainali katika NBA. Historia ilimbeba kuwa katika michezo miwili ya mwanzo hupata ushindi katika moja ya michezo jiyo. Lakini hali ilikuwa tofauti alfajiri ya kuamkia leo ule Oakland nyumbani kwa Golden State Warriors katika uwanja wa Oracle. Golden State Warriors iliendelea kuonyesha kuwa ni timu iliyokamilika kwani huku wafungaji wake bora wawili Stephen Curry na Klay Thompson wakiendelea kuwa wakimya wachezaji wengine wameendelea kuibuka na kuibeba timu hiyo. Baada ya Shaun Livingston kuwa na mchezo bora wa kwanza na kuisaidia timu yake kuichapa Cleveland, leo alikuwa ni Draymond Green aliyeisaidia Warriors kuibuka na ushindi wa pointi 110-77 za Cleveland Cavaliers. Draymond Green alifunga pointi 28, pasi 5 na kudaka rebound 7. Stephen Curry alipata faulo nne mapema katika robo ya tatu hivyo kumbidi kukaa nje mpaka robo ya nne ambayo nayo hakucheza sana kwani tayari Warriors ...