CLEVELAND CAVALIERS YAUWAWA KINYAMA MBELE YA GOLDEN STATE WARRIORS. YAPOTEZAA MCHEZO WA PILI WA FAINALI.

Kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya fainali, Lebron James hakuwahi kupoteza michezo miwili mfululizo ya fainali katika NBA. Historia ilimbeba kuwa katika michezo miwili ya mwanzo hupata ushindi katika moja ya michezo jiyo.

Lakini hali ilikuwa tofauti alfajiri ya kuamkia leo ule Oakland nyumbani kwa Golden State Warriors katika uwanja wa Oracle. Golden State Warriors iliendelea kuonyesha kuwa ni timu iliyokamilika kwani huku wafungaji wake bora wawili Stephen Curry na Klay Thompson wakiendelea kuwa wakimya wachezaji wengine wameendelea kuibuka na kuibeba timu hiyo.

Baada ya Shaun Livingston kuwa na mchezo bora wa kwanza na kuisaidia timu yake kuichapa Cleveland, leo alikuwa ni Draymond Green aliyeisaidia Warriors kuibuka na ushindi wa pointi 110-77 za Cleveland Cavaliers. Draymond Green alifunga pointi 28, pasi 5 na kudaka rebound 7.

Stephen Curry alipata faulo nne mapema katika robo ya tatu hivyo kumbidi kukaa nje mpaka robo ya nne ambayo nayo hakucheza sana kwani tayari Warriors walikuwa na uongozi wa zaidi ya pointi 20. Curry alimalliza mchezo akiwa na pointi 18 huku Klay Thompson akimaliza na pointi 17.

Lebron alikiri timu yake kushindwa wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya mchezo na kusema “kiukweli ni tumepigwa na walikuwa bora kutuzidi na sijaona eneo lolote ambalo tumewazidi”. Sasa mwendelezo unahamia nyumbani kwa Cleveland kwa ajili ya mchezo wa 3 na 4.

Lebron alimaliza robo ya kwanza bila kufunga pointi yoyote huku akiwa na pasi 5. Lakini alimaliza mchezo akiwa na pointi 19, pasi 9 na rebound 8 huku pia akipoteza mpira mara 7 kitu ambacho amekubali kupokea lawama.

KUMBUKUMBU YA MOHAMMAD ALI

Kulikuwa na muda wa ukimya na utulivu katika kumuenzi na kumkumbuka moja ya wanamasumbwi bora kuwahi kuikanyaga ardhi, Mohammad Ali ambaye alifariki wiki hii. Picha zake na video zilionyeshwa katika ubao wa matokeo kabla ya kuimbwa kwa wimbo wa Taifa.

REKODI

Warriors imeifikia rekodi ya 1995-96 iliyowekwa na Chicago Bulls ya kushinda michezo 87 kwa ujumla kwa msimu mmoja. Warriors walikwishavunja rekodi ya kushinda michezo 73 mapema msimu huu.

Kocha Steve Kerr anaungana na Phil Jackson kama makocha pekee walioshinda michezo 30 kati ya 40 ya mwanzo ya hatua ya mtoano.

Lebron James amefanikiwa kucheza mchezo wake wa 194 wa hatua ya mtoano hivyo kufika katika nafasi ya kumi na kuwaondoa Karl Malone na Danny Ainge waliokuwa wamecheza michezo 193.

Lebron James pia amemshusha John Stockton kutoka katika nafasi ya nne kwa kufanikiwa kupokonya mipira mara nyingi zaidi katika historia ya hatua ya mtoano ya NBA. Stockton alikuwa amepokonya mara 338.

HIGHLIGHTS

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA