ITALY IMEIVUA SPAIN UBINGWA WA ULAYA


Baada ya kufahamika kuwa Italy itacheza dhidi ya Hispania, wengi walikuwa wakiihurumia The Azzurri.

Kabla ya kufuzu hatua ya 16 bora, Italy imaliza kama kinara wa Kundi E na walionekana kuwa ni kikosi bora kwenye michuano hii baada ya kuilaza Ubelguji pamoja na Sweden.

Antonio Conte alizawadiwa kukutana na mabingwa mara mbili wa Ulaya kikosi chenye wachezaji bora wa muda wote.

Ulikuwa ni uwezo binafsi wa golikipa wa Hispania David De Gea uliosaidia kupunguza idadi ya magoli.

Kama alivyofanya kwenye timu yake ya Manchester United, De Gea alikuwa muhimili muhimu kwenye timu yake kwa kuokoa michomo kadhaa ya waitaliano kwenye vipindi vyote vya mchezo huo wa 16 bora ya michuano ya Euro 2016.

Italy wangeweza kupata ushindi wa zaidi ya magoli 2-0.

Giorgio Chiellini na Graziano Pellewalifunga magoli huku Gianluigi Buffon akilinda vema nyavu zake lakini timu ya Italy ilifanya kweli katika pambano hilo.

Kipigo hicho kinaacha wengi wakiamini huo ndiyo mwisho wa Vicente Del Bosque. Lakini pia inaonekana licha ya kuwa ni mwisho wa VDB, Andres Iniesta na David Silva huenda nao pia wakaamua kuachana na timu ya taifa.

Italy sasa itakutana uso kwa uso na timu ya taifa ya Ujerumani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA