Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UCHAMBUZI WA JOSE MOURINHO KWA NAMBA

UCHAMBUZI WA JOSE MOURINHO KWA NAMBA

Picha
Jose Mourinho ni kama tayari vile amemalizana na Manchester United isipokuwa ni suala la wakati kufika na kutangazwa tu kuwa kocha mpya wa ‘Mashetani Wekundu’. Licha ya Van Gaal kuwapa United kombe la FA, lakini hakufanikisha kuleta furaha ile ambayo mashabiki na viongozi wa klabu hiyo walitaraji kuipata kama ambavyo walikuwa wakipata katika utawala wa Sir Alex Ferguson. Van Gaal hana tayari ameshafungashiwa virago na nafasi yake itachukuliwa na Mreno huyo mwenye maneno na mbwembwe nyingi. Van Gaal amejitilia ugumu mwenyewe kutokana na kushindwa kuipa ndoo ya EPL United, lakini vile vile kushindwa kuipa nafasi ya kucheza michuano ya UEFA mwakani kitu ambacho kimekuwa ni fedheha kubwa kwa mashabiki hasa ukizingatia historia, umaarufu na ukubwa iliyonayo klabu yao. Uvumilivu umeonekana kuwashinda na sasa wanaamua kumkabidhi mikoba Mourinho ambaye mara zote amekuwa ni kocha wa makombe tu. Ikumbukwe kuwa Mourinho alishawahi kufanya kazi chini ya Van Gaal akiwa kocha msaidi...