Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Tiffah Wapima Sauzi

Diamond, Tiffah Wapima Sauzi

Picha
Mtoto Latifah Nasbu ‘Tiffah Musa Mateja, AMANI DAR ES SALAAM! Hii ni EXCLUSIVE stori! Kufuatia kelele kibao kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, yaani Latifah ‘Tiffah’ aliyemzaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ si wa nyota huyo, hatimaye, jamaa ameamua kupima vinasaba ‘DNA’ (DeoxyriboNucleic Acid). ISHU ILIKUWA AFRIKA KUSINI Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Diamond aliamua kutekeleza mpango huo nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako aliamini hakuna ‘macho mengi’ ya watu, hususan mapaparazi. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ SIKIA HII “Jamani mimi nataka niwape stori ambayo ni ya uhakika. Hivi mnajua kwamba Diamond aliamua kwenda Sauzi kupima DNA yake na mtoto wake Tiffah? “Kutokana na manenomaneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisufigisu, akamwambia Zari waende wakampime D...