Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wabunge Waibana serikali Matukio ya Mauaji Mwanza

Wabunge Waibana serikali Matukio ya Mauaji Mwanza

Picha
WAKATI matukio ya mauaji ya kikatili yakiendelea kuripotiwa kwenye maeneo mbalimbali nchini, Bunge limeitaka serikali kukomesha kadhia hiyo mara moja ili kuepusha maafa zaidi kwa watu wasio na hatia. Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alitoa tamko hilo bungeni mjini Dodoma juzi wakati akitoa mwongozo kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Mollel.    Mbunge huyo alisimama na kuomba Mwongozo wa Spika akiitaka serikali itoe kauli kuhusu kuwapo kwa matukio ya mauaji hayo.    "Mheshimiwa Naibu Spika, nasimama kwa Kanuni ya 68(7), lakini vilevile nakuu kupitia Ibara ya 14 ya Katiba ya Tanzania ambayo inasema kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria," Amina alisema.    "Kumekuwapo na matukio yanayotokea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hasa mikoa ya Manyara na Mara. Na hata jana (Jumatano) kulifanyika mauaji ya familia moja, baba na mama wamekatwakatwa mapanga na cha kusikitisha zaidi, huyo ma...