AU yatakiwa kusimamisha mauaji na mapigano Sudan Kusini
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeutaka Umoja wa Afrika (AU) kuchukua hatua za makusudi ili kusimamisha umwagaji wa damu za raia wasio na hatia huko Sudan Kusini.Ripoti mpya ya Human Rights Watch imewataka viongozi wa AU kuanzisha koti maalumu za kusikiliza kesi za jinai zinazodaiwa kufanywa na maafisa usalama wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika hususan katika eneo la Western Equatoria.Bekele, Mkurugenzi wa shirika hilo barani Afrika amesisitiza udharura wa kuchukua hatua za haraka kusimamisha mapigano hayo, ambayo kwa sasa yameanza kuenea katika maeneo mengine haswa upande wa magharibi mwa nchi. Kadhalika Human Rights Watch imeutaka Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo vya silaha wapiganaji wa pande zote zinazohusika katika mgogoro wa Sudan Kusini.Hii ni katika hali ambayo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International (AI) limelituhumu jeshi la Sudan Kusini kwamba limefanya uhalifu wa kivita kwa kuwakosesha pumzi kwa makusudi makumi ya ra...