Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Auawa Kwa Kuchomwa Visu Akituhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mtalaka Wake

Auawa Kwa Kuchomwa Visu Akituhumiwa Kutoka Kimapenzi na Mtalaka Wake

Picha
Mkazi wa Kijiji cha Chala B, Tarafa ya Chala wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, Moses Nambasita (48) ameuawa kwa kuchomwa visu kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Akisimulia mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Vincent Mwanambuu alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni baada ya kuvamiwa na kijana mmoja alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda nyumba jirani, alishambuliwa kwa kuchomwa visu. Mwanambuu alisema baada ya kupata taarifa hizo alitoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi Chala, askari walifika na kuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi na kuanza msako dhidi ya mtuhumiwa. Akielezea chanzo cha mauaji hayo, Mwanambuu alisema mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Nambasita ana uhusiano na mtalaka wake, ambaye walikuwa wameachana kipindi kirefu. Alidai kuwa kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alipeleka shauri la ugoni katika Mahakama ya Mwanzo Chala. “Lakini kabla hata shauri hilo halijamalizika, tunashangaa kuona mtuhumiwa ameamua kujic...