Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Uchovu isiwe sababu ya kunyimana ‘chakula cha usiku’

Uchovu isiwe sababu ya kunyimana ‘chakula cha usiku’

  Wanaume Ndani ya maisha ya ndoa, muda wowote mwenzako anapohitaji penzi hutakiwi kumkatalia kwa kuwa wewe ndiye daktari wake na kumkubalia kwako ni sawa na kumtibu ugonjwa ambao ungeweza kuyaathiri maisha yake. Hata hivyo, asilimia kubwa ya wanandoa wanatajwa kufanya tendo la ndoa wakati wa usiku. Usiku wa saa ngapi? Hiyo itategemea na wanandoa husika. Lakini sasa inaelezwa kuwa wanandoa wanaofanya kazi ni vigumu sana kulifurahia tendo la ndoa kwa kulifanya usiku. Hii ni kwa sababu, muda huo kila mmoja anakuwa amechoka kutokana na mihangaiko ya siku nzima. Usiku ni tatizo? Wanaume wengi wakati wa usiku ndiyo wanautumia kutafakari juu ya maisha, pia ni wakati ambao wanakuwa wamechoka hivyo wanaweza kukosa mshawasha wa kukutana na wake zao. Ukijaribu kufuatilia utabaini ndoa nyingi ziko kwenye migogoro chanzo kikiwa na wanawake kutopatiwa haki zao za ndoa. Wanaikosa haki hiyo kwa kuwa muda ambao waume zao wanatakiwa kuwapa ‘mambo’, wanakuwa hoi. Mbaya zaidi baadh...