SABABU ZA CHINA KUPIGA MARUFUKU HUDUMA ZA KAMPUNI YA APPLE
RACHEL GABAGAMBI Nchi nyingi duniani zimeridhia kupitisha Sheria ya Makosa ya Mtandao, lengo kuu likiwa ni udhibiti wa uhalifu mitandaoni na kuendelea kuboreshwa teknolojia kadri inavyoendelea kukua na kubadilika kutokana na kizazi na kizazi. Nchini Tanzania Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015 iliibua mijadala huku ikipingwa na wamiliki wa wadau wa masuala ya habari wakidai inawakandamiza katika kifungu cha 7(2b) kinachosema “Mpokeaji wa Ujumbe anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa jinai. Mfano mtu akikutumia ujumbe aliotumiwa na wewe ukaupokea na wewe uliyeupokea utakuwa umefanya kosa la jina i”. Wadau wa Vyombo vya Habari na Wanaharakati walipaza sauti zao juu ya uwepo wa sheria hii ambavyo kimsingi inalenga kufifisha uhuru wa kutoa na kupokea habari kama ambavyo vifungu vya 31 mpaka 35 na 39 mpaka 45 vikielekeza kuwa mmiliki wa mtandao wa kijamii au mtoa huduma, pale anapobaini kosa na akalitoa na akawa kwenye mk...