Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Haya ndio maeneo hatari kwa dawa za kulevya Dar

Haya ndio maeneo hatari kwa dawa za kulevya Dar

Picha
WAKATI Rais Dk. John Magufuli, akitangaza vita dhidi ya dawa za kulevya, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini maeneo hatari zaidi yanayoongoza kwa uuzaji wa dawa hizo. Imefahamika kuwa maeneo hayo yaliyopo jijini Dar es Salaam, yamekithiri kwa biashara hiyo haramu inayoangamiza nguvu kazi ya taifa, hususan vijana, huku wauzaji na watumiaji wa dawa hizo, wakijiwekea ulinzi na kutoa vitisho kwa wananchi na askari. Uchunguzi huo pia umebaini kuwa baadhi ya vigogo waliofungwa kwa tuhuma za kuhusika na biashara hizo, wamekuwa wakiendesha biashara hiyo wakiwa gerezani. Imeelezwa kuwa, wamekuwa wakiwatumia baadhi ya ndugu na marafi ki zao wanaowatembelea gerezani, kuwapa maagizo ya namna ya kusimamia shughuli zao. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, uchunguzi huo umebaini namna ambavyo baadhi ya wafanyabiashara hao wanavyotumia mbinu za hali ya juu kuingiza dawa hizo nchini. Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya utoaji mizigo kwenye Uwanja wa Ndege...