Ester Bulaya Atamba 'Nitaendelea Kumgaragaza Wasira Ubunge wangu si Wakuchakachua'
Mbunge wa Bunda Mjini, mkoani Mara, Esther Bulaya (Chadema), ametamba kuwa ataendelea kumshinda mpinzani wake kisiasa, Stephen Wasira (CCM), kwa madai kwamba alipata ubunge huo kihalali. Bulaya alisema hayo jana ikiwa ni siku moja tangu kutupwa kwa rufaa ya wanachama wa CCM waliokuwa wakipinga ushindi wa mbunge huyo alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Wassira na wagombea wa vyama vingine. Mbunge huyo aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake kuwa, alimshinda Wasira kwa wananchi, akamshinda kisheria, lakini hakuridhika akakata rufaa na ameendelea kumshinda. "Kama ana mpango wa kukata rufaa nyingine aende akate tu, lakini akumbuke kuwa nitaendelea kumshinda tu kwa sababu ubunge wangu sio wa kuchakachua bali nimeupata kutokana na kura za wananchi wa Bunda Mjini," alisema Bulaya na kuongeza: "Siku zote nimekuwa nikisema kuwa waliofungua kesi sio wanachama wa CCM bali ni Wasira mwenyewe, ndio maana akawa mkali kupigwa picha na waandishi il...