Polisi Waua Majambazi Wawili Mkoani Mwanza...... Walikuwa Wakitaka kuiba Nyumbani kwa Mfanyabiashara wa Madini
Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka Said. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Augustino Senga alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa 5:30 usiku katika Mtaa wa Kigala Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela. Alisema katika tukio hilo polisi walikamata silaha moja na risasi 21. Senga alisema majambazi hao waliokuwa wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 hawajafahamika majina wala makazi yao. “Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuwapo kwa majambazi yanayokusudia kuvamia kwa mfanyabiashara huyo, tuliweka mtego eneo la tukio ndipo majambazi hayo yalikuja yakiwa kwenye gari jeusi majira ya saa tano usiku,” alisema Senga. Katika tukio jingine, Wakazi wa stendi mpya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Daudi Joseph (32) na Magashi Mzee wameuawa kwa kup...