Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kigoma Zaongoza kwa Umasikini wa Kipato

Mwanza, Kagera, Kigoma Zaongoza kwa Umasikini wa Kipato

Picha
PAMOJA na maendeleo yaliyotokana na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania na kupungua kwa umasikini wa mahitaji ya msingi, serikali imeainisha mikoa mitano iliyokithiri kwa umasikini wa kipato. Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema mkoa unaoongoza ni  Kigoma ambao wakazi wake asilimia 48.9, wanakabiliwa na umasikini uliokithiri wa kipato. Mikoa mingine yenye umasikini wa kipato kiwango chake katika mabano ni Geita (asilimia 43), Kagera (asilimia 39), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3).  Katika wilaya zilizokithiri kwa umasikini wa kipato, ni Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera, ambapo Dk Mpango alisema katika wilaya hizo, takribani asilimia 60 ya watu wake, wako chini ya mstari wa umasikini wa mahitaji ya msingi. Tathmini ya hali ya umasikini kimaendeleo iliyoainisha umasikini huo, imetumia takwimu za Sensa ya Watu ya mwaka 2012 na ...