CAG Kuanika Mafisadi Bungeni Leo Wakati Akiwasilisha Ripoti Yake
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo anawasilisha bungeni ripoti ya mwisho ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/15. Ingawa haijajulikana rasmi nini kilichomo ndani yake, baadhi ya watu waliohojiwa wanatarajia CAG kubaini mchwa wanaotafuna fedha za umma na namna ya kukabiliana nao. Aidha wengine wanatarajia taarifa ya hali bora zaidi ya usimamizi wa fedha za umma kuliko kipindi cha nyuma. Ripoti hiyo awali ilikuwa imepangwa kuwasilishwa bungeni mwishoni mwa wiki (Aprili 22) kabla ya kuahirishwa hadi leo. “Ni kweli CAG atawasilisha ripoti kesho (leo) bungeni, ” Naibu Katibu wa Bunge na Utawala, Joel Joel alithibitisha juu ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo. Miongoni mwa wabunge waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, wamesema wanatarajia CAG kuonesha mambo mazuri kwa maana ya taasisi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa fedha za umma lakini pia mambo mabaya. “Lazima ripoti itaibua madudu maana walizoea (watend...