Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ukawa waitwa kwa meseji

Ukawa waitwa kwa meseji

Picha
Dar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema hivi sasa hawataki kushtukizwa kuhusu tarehe ya uchaguzi wa kumpata meya wa jiji la Dar es Salaam na naibu wake, badala yake wapewe taarifa hiyo siku saba kabla. Msimamo huo unafuatia viongozi wa Ukawa kutumiwa ujumbe mfupi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sarah Yohana akiwataka wafike ofisini kwake kesho kuchukua majibu ya nini kinachoendelea juu ya uchaguzi huo ulioahirishwa mara tatu. Machi 4, mwaka huu madiwani wa Ukawa walivamia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kumshinikiza Yohana kuitisha kikao cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa meya na naibu wake. Hata hivyo, madiwani hao zaidi ya 20 hawakufanikiwa kuonana na Yohana aliyedai yupo nje ya ofisi kikazi, walimuachia maagizo ya kumtaka aitishe kikao hicho ndani ya siku saba. Maagizo hayo alipewa  Ofisa  Utumishi na Utawala, Iman Kasagara. Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Katibu wa Chadema Mkoa wa ...