DC Wa Kinondoni Ally Hapi Aanza Mapambano Dhidi Ya Watumishi Hewa, Abaini 89 Waliolipwa Zadi Ya Sh Bilioni 1.331
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja. Aidha, Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya ualimu na hivyo kutoa siku saba kwa maofisa utumishi wa wilaya hiyo, kuhakiki watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na hasara waliyosababisha. Hapi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza kuwa awali wakati akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna watumishi hewa 34 waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512. Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi walibainika watumishi hewa wengine 55 walioisababishia serikali hasara ya Sh milioni 619 na hivyo kufanya jumla ya hasara kuwa Sh 1,131,754,081. “Bado uhakiki wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunamaliza hili tatizo la watumishi hewa katika wilaya ya Kinondoni, awali walikuwa 34 lakini sasa wameon...