MSANII JUX ASIMULIA ALIVYOMNASA VANESSA MDEE
na hapo ndipo walipoanza kujenga taratibu mahusiano yao. Kupitia kipindi cha Mkasi Jux amesema kuwa yeye lengo lake kubwa lilikuwa ni kufanya wimbo ambao alipenda kumshirikisha msanii wa kike anayeweza rap hivyo Pancho Latino alimsikilizisha kazi za Vanessa Mdee na akamkubali na kuamua kufanya naye kazi. "Mara ya kwanza nimekutana na Vanessa Mdee Studio kwa Pancho Latino nilienda kufanya kazi pale na nikawa nahitaji msichana ambaye ni mzuri kwenye kurap ili nimshirikishe hivyo basi Pancho akaniambia kuna msichana yupo mzuri, akanisikilizisha kazi zake nikazipenda japo niliona kama mzungu sana na kumwambia Pancho huyu tutambadilisha kidogo, hivyo kesho yake nilipoenda studio nikakutana na Vanessa pale tukafanya kazi tulipomaliza ilibidi nimrudishe kwao kwani kipindi hicho alikuwa hana usafiri". Alisema Jux Jux aliendelea kusimulia na kusema kuwa walikuja kukutana siku nyingine kwenye show ambapo wote walialikwa na siku hiyo ndipo alipata nafasi ya kumuangalia vizuri na ku...