Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NAMBA 1 HADI 62 NA MAANA ZAKE KATIKA VPL 2015-16

NAMBA 1 HADI 62 NA MAANA ZAKE KATIKA VPL 2015-16

Picha
Na Baraka Mbolembole Mechi sita za ligi kuu ya kandanda Tanzania bara zitachezwa leo Jumamosi na siku ya kesho Jumapili katika miji tofauti. Kama ilivyo kawaida ya mtandao wako huu wa tawfiqmassin.blogspot.com leo tena tunakuja tofauti. Kumbuka ni timu sita tu kati ya 16 za msimu huu zimewahi kushinda ubingwa VPL. Yanga, Simba, Mtibwa, Coastal, African Sports na Azam FC. Nimekuchambulia ligi yote na kukuwekea katika mtindo wa namba kuanzi namba moja (1) hadi 62. Ni timu moja tu kati ya 16 zinazocheza Ligi kuu ndiyo itapata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Afrika hapo mwakani. Kwa mara ya kwanza katika historia bingwa pekee wa ligi ndiye atapaa kimataifa.Namba hii inamuwakilisha mlinzi namba mbili wa Azam FC, Shomari Kapombe ambaye amefunga magoli 8 katika VPL hadi sasa na kuwa kinara wa ufungaji upande wa wachezaji wa nafasi za ulinzi. Mlinzi huyo wa Taifa Stars amekosa michezo miwili iliyopita ya timu yake na atakosa pia michezo mitano ya mwisho ku...