Kitete cha simu ‘feki’ chaanza
BAADHI ya wafanyabiashara nchini mwameanza kupaza sauti kwamba, muda uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuzifungia mawasiliano simu feki ni mfupi, anaandika Dany Tibason. Hivi karibuni TCRA wameetoa taarifa kwamba ifikapo Juni mwaka huu, simu ambazo si halisi ‘feki’ hazitaweza kufanya kazi na kuwataka wananchi kuanza kuchunguza simu zao na kisha kurejesha walipozinunua ama kujiandaa kununua mpya na halisi. Placid Nkya, mmilikiwa wa duka la simu la ‘Kwa Pablo’ mkoani Dodoma akizungumza na Mwanahalisi Online ameiomba serikali kuongeza muda wa kuzima simu feki kwani muda uliotangazwa ni mfupi huku akidai Watanzania walio wengi hawana elimu ya kutosha. Amesema, wananchi wengi wamekuwa wakinunua simu maarufu kama ‘za kichini’ kutokana na kuwa ni za gharama nafuu na hivyo walionunua kuingia hasara. “Kwao ni hasara kwa kuwa, bado simu inatumika na wala haijaharibika lakini mtu anatakiwa kununua nyingine. Kwanini wasianze kudhibiti k...