Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HAWA HAPA NDIO WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA KIKE BBC 2016

HAWA HAPA NDIO WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA KIKE BBC 2016

Picha
Mchezaji wa Cameroon Gaelle Enganamouit ameorodheshwa kushindania tuzo ya BBC inayotolewa kwa mchezaji bora wa kike wa mwaka 2016. Enganamouit, huchezea klabu ya Sweden ya Eskilstuna United, na alikuwa kwenye timu ya Cameroon iliyofika hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia la Wanawake mwaka jana ambapo iliondolewa na China. Wengine wanaopigania tuzo hiyo ni kiungo wa kati wa Ufaransa Amandine Henry, kiungo wa kati wa Scotland Kim Little na wachezaji wa Marekani Carli Lloyd na Becky Sauerbrunn. Wanaoshindania tuzo: Gaelle Enganamouit (Cameroon, fowadi, 23) Amandine Henry (Ufaransa, Kiungo wa kati, 26) Kim Little (Scotland, Kiungo wa kati, 25) Carli Lloyd (Marekani, Kiungo wa kati, 33) Becky Sauerbrunn (Marekani, Beki, 30)