Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

Picha
Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi. Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013. Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel. Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga. Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size). Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, ...