DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR ES SALAAM LEO
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini. Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji. Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao. "Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye" alisema Makonda. Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua wali...