Mama Harmonize Amtilia Shaka Wolper
Jacqueline Wolper Massawe na mkwe wake, mama Harmonize. STORI: MUSA MATEJA, WIKIENDA DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa wa Wimbo wa Bado, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumtambulisha mchumba’ke, Jacqueline Wolper Massawe nyumbani kwao katika Kijiji cha Mahuta mkoani Mtwara, siri imevuja kuwa wakati wa zoezi hilo, mama mzazi wa jamaa huyo, anadaiwa kumtilia shaka mrembo huyo juu ya mwanaye na kumpa wosia mzito. Tukio la utambulisho huo lilifanyika nyumbani kwa akina Harmonize Mtwara mara baada ya jamaa huyo kutinga mkoani humo kwa shoo yake ya kwanza maeneo hayo tangu alipochomoka kimuziki. Ilielezwa kwamba, akiwa katika harakati hizo mapema siku ya tukio, Harmonize alikwenda nyumbani kwao na kumtambulisha Wolper kisha usiku wake akampandisha mama yake kumtambulisha kwa mashabiki na baada ya kumtambulisha Wolper ambaye ni staa wa Bongo Muvi. Rajab Abdulhan ‘Harmonize’na mama yake mzazi. Chanzo hicho ambacho kilishuhudia hatua kwa hatua ya matukio ...