Rais Magufuli Awaapisha Makatibu Tawala Wapya Wa Mikoa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi. Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi. Makatibu Tawala walioapishwa ni; Arusha - Richard Kwitega Geita - Selestine Muhochi Gesimba Kagera - Armatus C. Msole Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour Pwani - Zuberi...