CAG, Msajili wa Hazina Watofautiana Kuhusu Shirika la Pride
Wakati Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) akisema Pride (Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprises) ni shirika la umma, Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru anasema hana nyaraka zinazoonyesha shirika hilo kuwa la Serikali bali anajua kuwa ni asasi isiyo ya kiserikali (NGOs). Kauli hiyo ya Mafuru imekuja siku chache baada ya CAG kutoa ripoti ya ukaguzi wa hesabu za mwaka 2014/ 2015 ambayo inaeleza kwamba shirika hilo la utoaji mikopo ni mali ya Serikali. Kama ilivyo katika ripoti za mwaka 2013/ 2014, safari hii CAG amesisitiza kwamba Pride ilianzishwa Mei 5, 1993 chini ya Sheria ya Makampuni (CAP 212) kwa lengo la kutoa mikopo midogo kwa wajasiriamali. Ripoti zote mbili za CAG zinabainisha kwamba fedha za kuanzishia taasisi hiyo zilitoka Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) kwa makubaliano baina ya Serikali za Tanzania na Norway. Pia, Serikali ya Sweden ilijiunga kukifadhili chombo hicho mwaka 2001. Katika ripoti ya mwaka 2014/ 2015, CAG anasema kwa m...